Ukiacha wimbo wa Amazing Grace kuwa ndio wimbo maarufu Zaidi wa injili duniani, Lakini Shackles( Praise you) ndio wimbo wa injili ambao umesikilizwa mara nyingi Zaidi na wasikizaji wa nyimbo za injili duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa spotify "Shackles (Praise You)" uliyoimbwa na Mary Mary
umesikilizwa na kupata streams Zaidi ya milioni 146 kutoka kwenye mtandao wa Spotify pekee kufikia Februari 2025 hivyo kushirikia rekodi ya wimbo wa injili uliosikilizwa Zaidi duniani.
Wimbo huu ulitolewa kwa mara ya kwanza tarehe 29 Februari 2000, na uliandikwa na Erica Atkins, Trecina Atkins, na Warryn Campbell. Tangu kutolewa kwake, "Shackles (Praise You)" umeimbwa na kurudiwa tena na wasanii mbalimbali, na kuna angalau matoleo 14 yanayojulikana hadi sasa.
0 Comments