Rapa, Rare of Breed. ( Photo courtesy of Rare of Breed)
Muziki wa hip-hop wa Kikristo umekua kwa kasi sana katika miaka ya hivi karibuni, na ukitaja majina makubwa ya wasanii wa muziki wa HipHop wa kikristo maarufu kama Christian rap basi huwezi acha kumtaja msanii maarufu Rare of Breed. Alizaliwa kama Rob Hardin mnamo Februari 28, 1990, huko Charlotte, North Carolina nchini Marekani, na amekuwa msanii maarufu katika aina hii ya muziki tangu alipo okoka na kumpokea Yesu mwaka 2011.
Maisha ya Rob yalikuwa na changamoto nyingi. Aliwekwa kwenye malezi ya watoto yatima akiwa na umri wa miaka 8 tu, na baadaye akajihusisha na matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya katika ujana wake wote, hali iliyosababisha matatizo ya kisheria na kufungwa gerezani akiwa na miaka 18. Mnamo 2011, alikutana na mtu aliyemwalika kanisani, jambo lililompelekea kukubali Ukristo kuukoka na kumpokea YESU kristo na hapo ndio Maisha yake yalipobadirika.
Rapa, Rare of Breed kushoto na Rapa Asap Preach Julia.
Baada ya kuokoka, Rob alikita kwenye muziki na kuanza kutumia rasmi jina la kisanii Rare of Breed. Alianza kuandika rasmi muziki wa hip-hop akichanganya na mizizi yake ya muziki wa country, na kuunda style ya kipekee iliyokuja kumpa umaarufu mkubwa sana duniani aliyoiita "GodTwang." Staili ambayo iliwagusa wenigi Duniani na kupata mitazamo tofauti.
Katika safari yake ya muziki, Rare of Breed ametoa jumla ya albamu 4 mpaka sasa, zikiwemo "GodTwang" ilitoka mwaka 2021, Godtwang2: Reloaded iliyotoka mwaka 2022, Godtwang 3: The next chapter iliyotoka mwaka 2023 na Take a Breath.
Hadithi ya Rare of Breed ni ushuhuda tosha wa namna Mungu anaweza kubadirisha maish ya mtu yeyote na kumtumia kwa namna ya kipekee kabisaa.
0 Comments