Ticker

6/recent/ticker-posts

Jimmy D Psalmist Aachia Wimbo Mpya "Lifter of Men"






Mwimbaji 
maarufu wa nyimbo za injili  kutoka nchini Nigeria na kiongozi wa ibada Jimmy Johnson  maarufu kama Jimmy D Psalmist, ameachia wimbo wake mpya uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu, “Lifter of Men,” ambayo imefuatiwa na video ya wimbo huo. Huu ni wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2025, ukiwa na ujumbe wenye imani na tumaini katika uwezo wa Mungu wa kutenda miujiza.

Wimbo huo wenye nguvu kiroho unatangaza imani kwa Mungu, ukionyesha uwezo wake wa kufanya yasiyowezekana. Kwa maneno kama, “Lifter of Men, is there anything You cannot do? What is impossible with men is possible with You,”wimbo huu unawahamasisha na kuwatia nguvu wasikilizaji kumtumainia Mungu kwa kila hali ya maisha.


Akizungumzia wimbo huo, Jimmy D Psalmist alisema: “Wimbo huu ni ukumbusho kwamba haijalishi mzigo wa maisha ni mzito kiasi gani, Mungu daima yuko tayari kutuinua. Amefanya hivyo hapo awali, na atafanya tena.”

“Lifter of Men” unafuata wimbo wake uliopokelewa vyema, “Jesus Oyoyooh,” ulioachiwa Novemba 2024. Wimbo mpya unapatikana sasa kwenye Apple Music, Spotify, Boomplay, na majukwaa mengine ya muziki mtandaoni.


Jimmy D Psamist ambaye  jina lake halisi anaitwa Jimmy Johnson kutoka nchini Nigeria amekuwa sauti kubwa katika tasnia ya muziki wa injili Afrika na Duniani kupitia albamu kadhaa, zikiwemo Mighty Man of War (2016), Consuming Fire (2018), Indomitable (2020),na Jesus Reigns (2021).

 



Post a Comment

0 Comments