Ticker

Jackson Paul Aachia Wimbo Mpya "Namwamini" Akimshirikisha Minister Paul Clement




Dar es Salaam, Tanzania – Mtumishi wa Mungu na mwanamuziki wa injili kutoka Tanzania, Jackson Paul, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa Namwamini, akimshirikisha mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili, Minister Paul Clement. Wimbo huo umetolewa leo, Jumamosi, na unapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali, ikiwemo YouTube na Instagram ya Jackson Paul.


Akizungumza na Gospel Connect TZ, Jackson Paul amesema kwamba Namwamini ni wimbo unaoelezea imani, matendo, na miujiza ya Yesu Kristo. Amebainisha kuwa ilikuwa mipango ya muda mrefu kushirikiana na Minister Paul Clement, na sasa mashabiki wake wanapaswa kutarajia mambo makubwa zaidi kutoka kwake katika siku zijazo baada ya wimbo huu kupokelewa vizuri na mashabiki.


Kwa mujibu wa maoni kutoka YouTube channel ya Jackson Paul, video ya wimbo huo tayari imepokea maoni chanya kutoka kwa mashabiki wa muziki wa injili. Pia, kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo amewashukuru mashabiki wake kwa sapoti na kuwataka waendelee kufuatilia kazi zake zinazokuja.


Kwa habari zaidi kuhusu wimbo huu, Namwamini na shughuli zote za muziki za Jackson Paul, mashabiki wanaweza kufuatilia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

 

Post a Comment

0 Comments